Casemiro amshangaza Manqoba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Aug 2026
Casemiro amshangaza Manqoba

Juzi Yanga ilianza vyema kampeni ya kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa sita mfululizo ikiichapa Namungo Fc mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

Katika mchezo huo Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi alimuanzia kiungo kinda Abdulnasir Mohamed Abdallah 'Casemiro' akicheza kwa dakika 65.

Akizungumza baada ya mchezo huo Manqoba alimpa kongole kiungo huyo kwa kile alichoonyesha katika mchezo huo.

Baada ya kile kilichotokea kwenye Yanga Day ambapo Casemiri alisababisha Aigles Du Congo kufunga bao la pili kufuatia kupoteza mpira eneo la hatari, Manqoba alihitaji kumpa nafasi nyingine ili kumuonyesha kuwa anamuani na kwa hakika hakumuangusha.

"Kijana amecheza vizuri sana. Nadhani amekamilisha pasi kwa zaidi ya asilimia 90%, kiulinzi alikuwa vizuri pia. Kiufupi nilivutiwa sana na nilifurahi sana kwasababu kama unakumbuka amecheza mchezo huu baada ya kutoka kwenye mchezo ambao goli lilifungwa kutokana na makosa yake."

"Nilitakiwa kumuonesha imani na ninaamini kabisa kwamba hapa Yanga imeongeza mchezaji kwenye kikosi na kutokana na alichotuonesha basi hata siku nyingine akipangwa, watu hawawezi kuuliza kwanini huyu?"

"Nilimtoa kwasababu alichoka wala si kwamba alikuwa anacheza vibaya. Kiukweli uwezo wake mchezoni na uelewa wa nini kinatakiwa kufanyike wapi kwa kijana mdogo kama yeye, inanishangaza sana," alisema Manqoba

Casemiro alitua Yanga msimu uliopita akitokea klabu ya Mlandege Fc ya visiwani Zanzibar. Msimu uliopita hakupata nafasi sana lakini msimu huu amelishawishi benchi la ufundi na huenda akatumika katika mechi nyingi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’