Yanga kutambulisha mchezaji mpya KMC Complex

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Aug 2026
Yanga kutambulisha mchezaji mpya KMC Complex

Klabu ya Yanga imeandaa hafla maalumu ya utambulisho wa mchezaji wao mpya katika dirisha hili kuelekea msimu wa 2026-27 ambapo utambulisho huo utafanyika apo kesho katika uwanja wa KMC jijini Dar es salaam.

Kupitia mkutano na wanahabari Meneja habari na Mawasiliano wa Yanga Ally Shaban Kamwe amesema kuwa utambulisho wa mchezaji huyo utaanza majira ya saa kumi jioni na atakuwa nyota wa mwisho kutambulishwa katika Timu hiyo.

Aidha sambamba na ilo Kamwe amewafahamisha Wanayanga kuwa hafla hiyo itakuwa na kiingilio Cha elfu mbili ambapo mashabiki na wadau wa timu hiyo watalipia katika mageti ya uwanja huo unaopatikana Mwenge , Kinondoni Jijini Dar es salaam.

“Kesho Yanga Sc tuna mchezo wetu wa kwanza wa ligi ambao tunacheza Ruangwa dhidi ya Namungo Fc ila kesho tutakuwa na hafla yetu ambayo itafanyika kwenye uwanja wa KMC”

“Kwa ukubwa wa tukio la kesho tutakuwa na mchezaji wetu mpya kwenye uwanja wa KMC kwenye tukio kubwa la utambulisho wa mchezaji huku tukiwa tunasubiri mechi yetu ambayo tutaenda kuitaza tukiwa uwanja wa KMC”

“Hii itakuwa mara ya kwanza Afrika kumtambulisha mchezaji mkubwa kwenye ligi yetu kwa kumtambulisha mchezaji wetu mpya” 

“Utaratibu wa utambulisho wa kesho tumeamua kuweka kiingilio ambacho kitakufanya umuone mchezaji wetu kwenye utambulisho huu kwa kulipia shilingi 2000/= kuanzia saa 10:00 jioni mageti yatakuwa wazi uwanja wa KMC”

“Kwa wanachama wa Black kadi tunawakaribisha uwanjani na watakaa eneo la VVP na kupata nafasi ya kusainiwa jezi yako na mchezaji unayemtaka na kupiga picha”

“Sisi Yanga pesa yetu ya usajili ipo kwenye mfuko wa Shati wa GSM maana yake angeweza kufunga msimu kimya kinya ila akaona lazima awape furaha nyingine mashabiki wa Yanga Sc kwa kushisha usajili mwingine mpya”

“GSM amesema hela ipo kwaajili ya matumizi sio kuzifungia ndani, kwahiyo njooni kesho uwanjani kuja kushuhudia furaha ya wananchi kwenye mchezo wetu wa kwanza wa ligi kuu tukiwa uwanja wa KMC,” alitamba Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
5h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’