Wakati Wananchi wakiendelea na shamrashamra za Ngao ya Jamii, kuna uwezekano mkubwa msimu ujao hawatakuwa na kiungo wao mshambuliaji mahiri Allan Okello baada ya uongozi wa Yanga kuthibitisha kupokea ofa kubwa mbili kwa ajili ya mchezaji huyo.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema klabu imepokea ofa mbili kutoka Afrika Kaskazini kutoka klabu za Wydad CA na AS FAR zote kutoka Morocco.
Kamwe amesema uongozi wa Yanga utafanya tathmini ya ofa hizo kabla ya kuamua kama wamruhusu Star Boy akatafut changamoto mpya huko Morocco au.
Okello hakuwa sehemu ya kikosi kilichoanza mchezo dhidi ya Simba jana akiingia baadae kwenye kipindi cha pili.
Taarifa kutoka duru za usajili ni kuwa Yanga tayari imemrejesha kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki ambaye ni wazi anaelekea kuchukua nafasi ya Okello.
Yanga inahitaji ofa isiyopungua Tsh Bilioni 3 ili kumuuza Okello