Azam FC, Singida United zaunga tela kumuwania Tinocco

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jun 2018
Azam FC, Singida United zaunga tela kumuwania Tinocco
Vilabu vya Azam FC na Singida United zimeingia kwenye vita ya kumuwania mlinda lango wa Mtibwa Sugar Benedict Tinocco ambaye pia anawaniwa na Yanga.

Tinocco ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu yake ya Mtibwa, amekiri kuwa timu zote tatu ziko kwenye mazungumzo na uongozi wa Mtibwa.

"Suala la kutafutwa na vilabu hivyo lipo lakini shida inakuja kwamba mimi bado nina mkataba na timu yangu ya Mtibwa ndio maana hakuna mazungumzo yoyote kwa sababu bado nipo chini ya watu," Tinocco amenukuliwa na mtandao wa ShaffihDauda

"Mkataba inabidi uheshimiwe, sina uamuzi wowote kwa sababu mimi si mchezaji huru nasubiri mazungumzo yao kama yataenda vizuri mimi nipo tayari kucheza popote kwa sababu mpira ndio kazi yangu."

"Bado sijaambiwa mazungumzo yamefikia hatua gani kwa sababu ni mapema sana, naendelea kusubiri kila kitu kikiwa sawa wataniambia wameamua nini," amesema.

Licha ya kuhusishwa na Vumi-Ley Matampi, mlinda lango aliyemaliza mkataba kwenye klabu ya TP Mazembe, Yanga inasaka mlinda lango mwingine wa ndani.

Mkataba wa Benno Kakolanya umemalizika huku kukiwa hakuna uhakika kama Yanga itaendelea nae kutokana na kusumbuliwa na majeraha yaliyomfanya atumike mara chache msimu uliomalizika.

Matampi anadaiwa kuletwa nchini kuchukua nafasi ya Youthe Rostand ambaye msimu mmoja alioitumikia Yanga ameshindwa kulishawishi benchi la ufundi la timu hiyo.

Yanga pia inahusishwa na kipa wa Bandari ya kenya, Farouk Shikalo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’