Klabu ya Petro Atletico ya Angola imetangaza kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Laurindo Aurelio 'Depu'.
Depu ambaye aliitumikia Yanga kwa miezi sita tu, alisafiri jana kuelekea Angola kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wake.
Inaelezwa Yanga imeingiza takribani 1.3B kutokana na mauzo ya mshambuliaji huyo ambaye aliifungia Yanga mabao 14 katika muda mfupi aliowatumikia Wananchi.
Yanga imelazimika kumuuza Depu baada ya kujitosheleza eneo la safu ya ushambuliaji baada ya kuwasajili Cheick Ibrahima Toure, Peter Shalulile na Suleiman Mwalimu.
Mauzo ya mshambuliaji huyo pia yanaweza kuingozea nguvu Yanga katika maboresho zaidi ya kikosi, taarifa zinabainisha kuwa Wananchi hawajafunga hesabu za usajili kuna michakato inaweza kukamilishwa kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumamosi, saa 5:59 usiku.
