Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga SC, wameshtukiza katika soko la usajili asubuhi ya leo baada ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji Selemani Mwalimu 'Gomez'.
Usajili huo ulioratibiwa kwa siri kubwa na Rais wa Klabu hiyo, Injinia Hersi Said huko Zanzibar, umekuja kama 'sapraizi' nzito kwa wapenzi wa soka nchini, ikizingatiwa mchezaji huyo alikuwa mbioni kujiunga na mahasimu wao, Simba SC, alikocheza msimu uliopita kwa mkopo.
Mwalimu anajiunga na Yanga kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja akitokea klabu ya Wydad AC ya Morocco.
Juzi Simba ilimtambulisha Mwalimu kwenye Tamasha la SIMBA DAY na alitua Zanzibar kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii baina ya timu hizo.
ADVERTISE HERE