Kikosi cha Yanga kimewasili visiwani Zanzibar tayari kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.
Mchezo huo utapigwa Jumatano, August 12 katika uwanja wa New Amaan Complex, saa 2:30 usiku.
Yanga ndio mabingwa watetezi wa Ngao ya Jamii wakiitwaa msimu uliopita kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani zao hao mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Pacome Zouzoua akifunga bao pekee.
Kocha Mkuu wa Yanga Manqoa Mngqithi amewahakikishia kikosi chake kiko imara na wanakwenda kupambana katika mchezo huo kuhakikisha wanaibuka na ushindi.






ADVERTISE HERE