Achana matokeo ya mchezo dhidi ya Les Aigles Du Congo ambapo Yanga walipoteza kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kilele cha wiki ya Wananchi, kocha mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi aliutumia mchezo huo kimkakati zaidi.
Aliwapa nafasi wachezaji wake wengi akitumia kikosi tofauti kwenye kila kipindi. Lakini jambo lililowafurahisha wengi ni kuwaani vijana wawili kutoka timu ya vijana U20 Saleh Mahsen na Kazimoto.
Mohsen alianza kama beki wa kushoto kwenye kipindi cha kwanza huku Kazimoto akiingia nafasi ya beki wa kulia kwenye kipindi cha pili.
Mohsen ambaye kwenye kikosi cha Yanga U20 hutumika kama kiungo mshambuliaji, jana alin'gara katika nafasi ya mlinzi wa kushoto.
Ukizungumzia wachezaji waliopata alama nyingi kwenye tamasha hilo, Mohsen ni miongoni mwao.
Hiki ni kipaji ambacho kinakwenda kuinufaisha Yanga msimu huu kwani licha ya umri wake mdogo, ameonyesha kujiamini akikabiliana na wachezaji waliomzidi umri lakini wenye uzoefu mkubwa.