Klabu ya Bandari Tanzania SC inayoshiriki Ligi ya NBC Championship imetikisa soko la usajili kwa kumsajili aliyekuwa beki wa kushoto wa Yanga, Joyce Lomalisa Mutambala.
Beki huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mwenye umri wa miaka 33, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo.
Bandari Fc wamemsajili Lomalisa kuongeza uzoefu wa kimataifa na nguvu kwenye safu ya ulinzi.
Bandari Fc imepanda daraja kutoka Ligi ya Maendeleo (First League), inaonekana kudhamiria kufanya makubwa ligi ya Championship wakisaka tiketi ya kucheza ligi kuu.
Lomalisa aliitumikia Yanga kwa mafanikio misimu mitatu nyuma kabla ya kuelekea Angola ambako alizitumikia klabu kadhaa.
ADVERTISE HERE