Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga SC, wanatarajiwa kushuka uwanjani kukabiliana na miamba ya soka kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), klabu ya Aigles du Congo, katika kilele cha tamasha la Yanga Day (Wiki ya Wananchi) msimu huu wa 2026/2027.
Kilele cha tamasha hilo ambalo husubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini, kinatarajiwa kufanyika wikiend hii, Jumapili, Agosti 9, 2026, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Maandalizi kuelekea Tamasha hilo kubwa zaidi la burudani ndhini yamekamilika huku wapinzani wao Aigles du Congo wakiwa tayari wako nchini.
Yanga Day ni zaidi ya burudani ya soka kwani mashabiki watapata fursa ya kushuhudia utambulisho rasmi wa wachezaji wapya pamoja na benchi la ufundi.
Bado tiketi zinapatikana ambapo mzunguko ni TSh 20,000 na VIP ni TSh 100,000, huku tiket maalum za Royal zikiuzwa kwa TSh 300,000.
Aigles du Congo ni mabingwa wa msimu uliopita ligi kuu ya DR Congo ambapo msimu huu wamemaliza nafasi ya pili nyuma ya TP Mazembe. Ilianzishwa na mfanyabiashara na mwanasiasa mashuhuri nchini DRC, Vidiye Tshimanga Tshipanda, baada ya kununua leseni ya klabu ya Jeunesse Sportive de Kinshasa (JSK)
Waliweka kambi ya maandalizi yao ya pre-season nchini.