Dondoo za kombe la dunia : Egypt vs Uruguay

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jun 2018
Dondoo za kombe la dunia : Egypt vs Uruguay
Kikosi cha timu ya Taifa ya Misri kinashuka dimbani leo kucheza mchezo wa kwanza wa michuano ya kombe la dunia dhidi ya Uruguay huko Urusi.

Habari njema kwa Misri na Waafrika kwa ujumla ni kurejea kikosini kwa mshambuliaji Mohammed Salah aliyekuwa na hatihati ya kukosa mchezo wa ufunguzi kutokana na majeraha ya bega aliyopata May 26 kwenye mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kati ya Liverpool dhidi ya Real Madrid.

Misri imerejea kwenye michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza baada ya kukosa kwa miaka 28.

Mabingwa hao wa kihistoria wa Afrika watakuwa wanasaka ushindi wao wa kwanza kwenye michuano hiyo.

Kabla ya mwaka huu, Misri imewahi kufuzu kwa fainali za kombe la dunia mara mbili na haijawahi kushinda.

Kwa upende wa Uruguay, imekuwa ikishiriki michuano hiyo mara kwa mara.

Hata hivyo katika fainali sita zilizopita Uruguay imepoteza michezo yake yote ya Ufunguzi huku ikwa na rekodi ya kutopoteza mchezo dhidi ya timu za Afrika.

Misri na Uruguay zimewahi kukutana mara moja tu kwenye mchezo wa kirafiki mwaka 2006 ambao Uruguay ilishinda kwa mabao 2-0.

Baada ya Urusi kushinda kwa mabao 5-0 jana dhidi ya Saudi Arabia, timu itakayoshinda leo itakuwa imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda hatua ya mtoano kwani upo uwezekano mkubwa kwa Saudi Arabia kugawa alama tatu kwa timu zote kundi A.

Mchezo huo wa kukata na shoka unatarajia kuanza saa tisa Alasiri kisha kufuatiwa na mchezo mwingine wa kundi B kati ya wawakilishi wengine wa Afrika, Morocco dhidi ya Irani utakaoanza saa 12 jioni.

Saa tatu usiku kutakuwa na mchezo wa kwanza 'mkali' kati ya mabingwa wa Ulaya Ureno dhidi ya mabingwa zamani wa bara hilo Hispania.

Ureno itaongozwa na nahodha wake Cristiano Ronaldo ambaye huenda akakutana uso kwa uso na beki Sergio Ramos wanayecheza wote klabu ya Real Madrid.

Licha ya Hispania kumtimua kocha wao siku mbili kabla ya mchezo huo, tukio hilo halitarajiwi kuathiri kasi ya Hispania iliyosheheni wasakata kabumbu wenye vipaji vya hali ya juu.

Mkongwe na nahodha wa zamani wa Real Madrid, Fernando Hierro ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kuivusha Hispania kwenye michuano ya kombe la dunia baada ya kutimuliwa Julen Lopetegui aliyetangazwa kujiunga na Real Madrid kuchukua nafasi ya Zinadeine Zidane.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’