Hersi awataka walioiba Ngao ya Jamii 2025 wairudishe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Aug 2026
Hersi awataka walioiba Ngao ya Jamii 2025 wairudishe

Rais wa klabu ya Young Africans SC, Hersi Said, amewataka watu waliochukua Ngao ya Jamii 2025 kuirejesha, akisisitiza kuwa mataji ya soka yanapaswa kupatikana kwa ushindi wa uwanjani na si kwa njia nyingine yoyote.

Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama mapea leo, Hersi alisema tukio la kupotea kwa Ngao hiyo lilitokea wakati klabu hiyo ikiwa katika kipindi cha kusherehekea mafanikio yake.

β€œWakati tunasherekea ubingwa wetu, kuna watu wakaiba Ngao ya Jamii 2025. Kama kuna mtu analo alirudishe. Taji linashindaniwa uwanjani,” alisema Hersi.

Aliongeza kuwa Ngao hiyo ilitengenezwa nchini Tanzania, hivyo klabu hiyo tayari imechukua hatua ya kuagiza nyingine kutengenezwa.

β€œKwa bahati nzuri hii ilitengenezwa hapa hapa Tanzania, hivyo tumeagiza watutengenezee,” alisema.

Hersi pia alitoa wito wa moja kwa moja kwa waliohusika na kupotea kwa Ngao hiyo kuhakikisha wanairejesha, akisisitiza thamani ya ushindani wa haki katika mchezo wa soka.

β€œPia nichukue nafasi hii kuwaambia wale walioiba Ngao hii wairudishe. Rudisheni Ngao, taji hili linapatikana kwa kushinda uwanjani na sio kuiba,” alisema Hersi.

Yanga ilitwaa Ngao ya Jamii 2025 wakiifunga Simba bao 1-0 katika mchezo uliopigwa Septemba 16 2025 uwanja wa Benjamin Mkapa.

Download Xtra 90 App

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’