Hersi aweka hadharani mafanikio ya miaka minne Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Aug 2026
Hersi aweka hadharani mafanikio ya miaka minne Yanga

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Ally Said, ameweka hadharani mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake, akieleza kuwa klabu hiyo imeandika historia mpya ndani na nje ya Tanzania kupitia mataji, rekodi na mafanikio ya kimashindano.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Yanga, Hersi alisema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano kati yake, Kamati ya Utendaji, viongozi na wadau wote wa klabu.

Hersi alisema katika kipindi cha miaka minne, Yanga imefanikiwa kutwaa jumla ya makombe 16 katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, huku ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara nne mfululizo chini ya uongozi wake.

β€œKatika kipindi cha Miaka minne cha uongozi wangu, nikishirikiana na Kamati Tendaji, Yanga, tumeshinda Jumla ya makombe 16 ndani na nje ya nchi. Ligi Kuu ya NBC, Tanzania Bara, Mataji manne (4) na kuweka rekodi ya kubeba Ubingwa mara 5 mfululizo, ukijumlisha na mara moja tuliyobeba nikiwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano,” alisema Hersi

Aidha, alisema mafanikio hayo yameifanya Yanga kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara tano mfululizo, ukiwemo ubingwa mmoja aliouchangia akiwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano.

Mbali na mataji, Hersi alieleza kuwa Yanga imeweka rekodi bora katika Ligi Kuu kwa kucheza mechi 120, kushinda 101, kutoka sare 12 na kupoteza mechi saba pekee. Katika kipindi hicho, klabu ilikusanya pointi 315, ikifunga mabao 286 na kuruhusu mabao 51 pekee, ikiwa na tofauti ya mabao 235.

Katika Kombe la Shirikisho la CRDB, Hersi alisema Yanga imeandika historia nyingine kwa kutwaa taji hilo mara nne mfululizo. Pia alibainisha kuwa klabu imecheza mechi 28 katika kipindi cha miaka mitano, ikipoteza mchezo mmoja pekee huku ikisalia bila kufungwa katika mechi 27, ikifunga mabao 86, kufungwa 14 na kuweka rekodi ya clean sheet 20.

Hersi pia alikumbushia mafanikio ya Yanga kwenye mashindano mengine, akisema klabu imetwaa Kombe la Ngao ya Jamii mara nne kwa kuwafunga wapinzani wake wakuu, Simba na Azam, katika nyakati tofauti.

Kimataifa, alisema Yanga iliialikwa kushiriki michuano ya Toyota Cup nchini Afrika Kusini na kufanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kuifunga Kaizer Chiefs mabao 4-0. Pia, klabu ilitwaa ubingwa wa Rayon Day nchini Rwanda kwa kuichapa Rayon Sports mabao 3-1.

Akihitimisha hotuba yake, Hersi aliwashukuru viongozi wote aliowahi kufanya nao kazi, akiwapongeza kwa mchango wao katika mafanikio ya klabu na kuwatakia kila la heri kuelekea uchaguzi wa viongozi.

"Nitafurahi kama viongozi wote waliopo watarudi, lakini pia natambua kuwa kuna wanachama wengine wenye uwezo mkubwa wa kuiongoza Yanga. Kama kuna mgombea ambaye wanachama wanaona anafaa, wamchague. Mimi niko tayari kufanya kazi na mwanachama yeyote mwenye dhamira njema kwa maendeleo ya klabu yetu," alisema Hersi.

Download Xtra 90 App

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’