Ridhiwani Kikwete achukua nafasi ya Dk Mwigulu Nchemba Baraza la Wadhamini Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Aug 2026
Ridhiwani Kikwete achukua nafasi ya Dk Mwigulu Nchemba Baraza la Wadhamini Yanga

Klabu ya Yanga imefanya mabadiliko katika Baraza lake la Wadhamini baada ya Dk Mwigulu Nchemba kuomba kuachia nafasi yake kutokana na majukumu yake makubwa ya kitaifa kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Yanga, Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said, amesema Dk Mwigulu aliwasilisha ombi la kujiondoa katika Baraza la Wadhamini kwa hiari yake ili aweze kujikita katika kutekeleza majukumu aliyopewa na taifa.

Hersi amesema Kamati ya Utendaji ya Yanga ilipokea ombi hilo na kulijadili kabla ya kufikia uamuzi wa kumteua Ridhiwani Kikwete kuziba nafasi iliyoachwa wazi.

"Baada ya kupokea ombi la Dk Mwigulu, Kamati ya Utendaji ilikutana na kujadili suala hilo na hatimaye ikamchagua Mh. Ridhiwani Kikwete kuwa mjumbe mpya wa Baraza la Wadhamini," amesema Hersi.

Dk Mwigulu alikuwa mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wadhamini waliokuwa wakichangia katika ushauri na uongozi wa kimkakati wa klabu hiyo. Kuondoka kwake kunafuatia kuongezeka kwa majukumu yake ya kitaifa, hatua iliyolazimu kuachia nafasi hiyo ili kutoa fursa kwa uongozi mpya kuendelea kutekeleza majukumu ya baraza.

Kwa uteuzi huo, Ridhiwani Kikwete sasa anaungana na wajumbe wengine wa Baraza la Wadhamini katika kusimamia maslahi ya Yanga.

Hii hapa safu mpya ya Baraza la Wadhamini la Yanga;

Mwenyekiti:
Mheshimiwa George Mkuchika

Wajumbe:
1. Bi. Fatma Karume
2. Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete
3. Mheshimiwa Anthony Peter Mavunde
4. Mheshimiwa Abbas Tarimba

Download Xtra 90 App

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’