Leo ni Mkutano Mkuu na Uchaguzi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Aug 2026
Leo ni Mkutano Mkuu na Uchaguzi Yanga

Klabu ya Yanga leo inatarajia kufanya tukio la kikatiba ambapo Wanachama wake wanatarajiwa kufurika katika Ukumbi wa Super Dome uliopo Masaki jijini Dar es salaam, kushiriki Mkutano Mkuu wa Mwaka unaoenda sambamba na Uchaguzi Mkuu wa viongozi wapya.

Mkutano huo mkubwa uliopangwa kuanza rasmi majira ya saa 3 asubuhi ambapo wanachama watapata fursa ya kidemokrasia kuchagua safu mpya ya viongozi watakaogoza klabu hiyo kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ambaye anagombea nafasi hiyo kwa awamu ya pili, amewaalika Wanachama kwenye Mkutano huo ili kutumia haki yao ya kikatibu kwa kushiriki uchaguzi.

"Kamati ya Utendaji, tunapenda kusema kuwa kesho (leo) itakuwa siku ya kihistoria kwa klabu yetu. Ni mkutano wa kihistoria utakaofungua ukurasa mpya katika historia ya Yanga. Tunawashukuru sana wanachama na wapenzi wa Yanga kwa namna ambavyo mmeendelea kutuunga mkono katika kipindi chote cha uongozi wetu.”

“Wanachama watakaoshiriki uchaguzi wanapaswa kutambua kuwa hii ni siku muhimu sana kwa maslahi mapana ya klabu yetu. Tunakwenda kufanya mabadiliko kadhaa ya Katiba ambayo yataifanya klabu yetu kuwa katika mazingira bora na ya kisasa ya uendeshaji."

"Tunawasihi sana wafanye maamuzi sahihi yatakayofungua milango mipya ya maendeleo na mustakabali mzuri wa klabu yetu,” alisema Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’