Siku chache zilizopita, Kamati maalumu ya mpito inayoongozwa na Mwenyekiti Abbas Tarimba ilikutana kupanga mikakati ya kutekeleza majukumu waliyopewa.
Kamati hiyo iliundwa na Bodi ya Wadhamini ya klabu ya Yanga na kuridhiwa na wanachama wote katika mkutano mkuu uliofanyika Juni 10 ukumbi wa bwalo la Polisi, Masaki jijini Dar es salaam.
Jana Tarimba alieleza kuwa tayari wameanza majukumu yao na watayafanya kwa weledi mkubwa.
Kuhusu masuala ya usajili Tarimba amesema watashirikiana na Kamati ya usajili ya Yanga kwa kutumia utaratibu unaotumika sasa wa kusajili kimyakimya ili kuepuka hujuma.
Mbali na kufanya usajili kwa ajili ya msimu ujao, Yanga inapaswa kujaza nafasi tatu za wachezaji watakaoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho.

ADVERTISE HERE