Kikosi cha Yanga kimeendelea na maandalizi ya msimu wa 2026/27 leo wakicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Magereza Fc ya Dar es salaam na kuibuka na ushindi wa mabao 7-2 .
Mchezo huo ulikuwa ni sehemu ya programu ya kujiandaa na msimu mpya. Huo ulikuwa mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa Yanga tangu ilipoanza maandalizi ya msimu mpya wiki iliyopita.
Katika ushindi huo, Depu alikuwa nyota wa mchezo baada ya kufunga mabao mawili, huku mabao mengine yakifungwa na Boka, Kangwanda, Edmund, Okello na Casemiro.
Miongoni mwa waliochangia pasi za mabao ni Okello, Max, Shekh na Mpemba D.









ADVERTISE HERE