Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga watavaana na watani wao wa jadi, Simba SC ambao ni mabingwa CRDB CUP katika mchezo wa Ngao ya Jamii 2026 utakaochezwa Agosti 12, 2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Mchezo huo, unaoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), unatarajiwa kuashiria mwanzo rasmi wa msimu wa 2026/27.
Mtanange huo utakuwa ya kwanza kwa kocha mpya wa Yanga, Manqoba Mngqithi kuwaongoza Wananchi dhidi ya Simba katika mechi ya ushindani.
Mbali na kuwania Ngao ya Jamii, pambano hilo linatarajiwa kuwa kipimo muhimu cha utayari wa kikosi cha Yanga kuelekea msimu mpya wa mashindano baada ya mabadiliko ya benchi la ufundi.
ADVERTISE HERE