Kiungo mshambuliaji wa Yanga Allan Okello ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha mabingwa hao wa nchi ambao wanaendelea na maandalizi ya pre-season chini ya kocha Manqoba Mngqithi Avic Town.
Wakati wenzao wa ndani wakianza mazoezi wiki iliyopita, nyota wa kigeni waliingia rasmi kambini siku ya Jumatatu, Okello akiwa miongoni mwao.
Baada ya kuwasha moto msimu ulopita, matarajio ya mashabiki wa Yanga ni kuona msimu ujao Okello ataendeleza pale alipoishia.
Licha ya kutua kwenye dirisha dogo, msimu uliopita alimaliza akiwa mfungaji bora wa Yanga akifunga mabao 14 pia akitoa pasi nane za mabao.
Wakati huu anakwenda kuanza mwanzo wa msimu katika kikosi ambacho pia kimeongezewa nguvu kwa usajili mkubwa uliofanyika.



ADVERTISE HERE