Hersi afichua alivyomfuatilia Shalulile kwa miaka mitatu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jul 2026
Hersi afichua alivyomfuatilia Shalulile kwa miaka mitatu

Usajili wa mshambuliaji nyota wa Namibia, Peter Shalulile, kujiunga na Yanga haukuwa wa ghafla wala wa bahati mbaya. Rais wa klabu hiyo, Hersi Ally Said, amefichua kuwa alikuwa akifanya mazungumzo na mchezaji huyo kwa kipindi cha miaka mitatu kabla ya ndoto yake kutimia.

Akizungumza kuhusu safari ya kumpata Shalulile, Hersi alisema alianza kumshawishi mshambuliaji huyo muda mrefu uliopita, akimueleza mara kwa mara kwamba siku moja angevaa jezi ya Wananchi.

“Nimekuwa nikizungumza na Peter kwa miaka mitatu. Kila mara nilikuwa namwambia, ‘Siku moja utakuwa mchezaji wangu,’” alisema Hersi.

Hersi pia alifafanua kuwa Shalulile alikuwa mchezaji huru, jambo lililompa nafasi ya kufanya uamuzi wake mwenyewe bila vizuizi vya mkataba. Licha ya kuvutiwa na klabu zenye uwezo mkubwa kifedha kama Pyramids FC ya Misri na Raja Casablanca ya Morocco, mshambuliaji huyo aliamua kuichagua Yanga kutokana na maono na mradi wa klabu hiyo.

“Peter alikuwa mchezaji huru, hivyo uamuzi ulikuwa wake kabisa. Kulikuwa na klabu zilizompa fedha nyingi zaidi kuliko sisi, lakini alichagua mradi wetu,” aliongeza.

Mwenyekiti huyo wa umoja wa klabu barani Afrika (ACA) pia amebainisha kuwa hatua ya mwisho ya mazungumzo ilichukua wiki mbili, ambapo alijikita kumshawishi kuhusu mazingira ya klabu, sapoti ya mashabiki na malengo makubwa ambayo Yanga imejiwekea kwa miaka ijayo.

“Ilinichukua wiki mbili kumshawishi. Nilimwambia hii si suala la kusaini mkataba tu, bali ni kuhusu mazingira, sapoti ya mashabiki na kile tunachotaka kufanikisha pamoja,” alisema.

Hii sio mara ya kwanza kwa Hersi kufanikisha usajili wa mchezaji mwenye 'profile kubwa' licha ya mazingira kuonyesha kama ni jambo lisilowezekana.

msimu wa 2022/23 alimsajili kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki kutoka klabu ya Asec Mimosas katika usajili ambao hakuna aliyeamini hadi pale alipotambulishwa saa 8 usiku.

Licha ya utambulisho wa Aziz Ki kufanyika usiku wa manane, mashabiki wa Yanga na wadau wa soka walikesha wakisubiri tangazo hilo la Yanga ili kuthibitisha kama Aziz Ki ni kweli ametua kwa Wananchi.

Bado Injinia Hersi ana 'surprise' mbili za wachezaji wa kigeni kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’