Unaambia huko Avic Town hakuna kulala! wachezaji wa Yanga wanatumika kwelikweli katik maandalizi ya kikosi cha mabingwa hao wa nchi kuelekea msimu mpya wa mashindano 2026/27.
Meneja wa habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amefichua kuwa kocha Manqoba Mangqithi ameandaa mfululizo wa program za mazoezi zinazoanza asubuh hadi saa 8 mchana.
Kamwe amebainisha kuwa asubuhi kunakuwa na mazoezi ya Gym na kisha kufuatiwa na program nyingine za kimbinu kabla ya kuelekea uwanjani kukamilisha program za kucheza mpira.
"Manqoba ni kocha anayependa mpira uchezwe hivyo muda mwingi sana unatumika kwa maandalizi ya kimbinu uwanjani," alibainisha Kamwe.
Leo ikiwa siku ya nne ya pre-season, wachezaji wa kigeni wataanza kuonekana mazeozini. Wachezaji hao walipewa siku zaidi za kuripoti kambini kwa kuwa wengi walisafiri nje ya nchi.



