Kiungo mshambuliaji Shekhan Khamis jana alianza rasmi kuitumikia Singida Black Stars kwenye mchezo wa kombe la Kagame dhidi ya Jamus Sc, alishuhudia waajiri wake wapya ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo wakipoteza kwa mabao 2-0.
Shekhan amejiunga na Singida BS kwa mkopo wa msimu mzima akitokea klabu ya Yanga.
Bado ana mkataba wa muda mrefu na Yanga, ametolewa kwa mkopo ili akapate nafasi zaidi kucheza na kulinda kiwango chake.
Shekhan alitumika kwa dakika zote 90 kwenye mchezo huo uliopigwa uwanja wa Pele, Kigali
ADVERTISE HERE