Yanga itafunga vipi hesabu za Wata Pleya?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
25 Jul 2026
Yanga itafunga vipi hesabu za Wata Pleya?

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema nafasi mbili za wachezaji wa kigeni zilizobaki zitajazwa na ma 'Wata Pleya' wengine.

Wakati akitangaza usajili wa nyota watatu wa kigeni jana, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alidokeza kuwaa wamesajili wachezaji watano ambao wataungana na wachezaji 7 waliobaki kukamilisha idadi ya wachezaji 12.

Mapema leo Yanga ilithibitisha kuwa mongoni mwa nafasi zilizobaki ni kiungo mkabaji na ndiye mchezaji anayefuata kwenye utambulisho.

Kamwe ametamba kuwa Yanga imemsajili mmoja wa viungo mahiri kwenye bara la Afrika akiamini anatua kumaliza changamoto eneo la kiungo mkabaji.

Kuhusu mchezaji wa pili, Kamwe amesema jina lake lipo miongoni mwa majina ya wachezaji wengi ambao wamehusishwa na tetesi za kujiunga na Yanga.

Miongoni mwa wachezaji waliohusishwa sana na Yanga ni pamoja na kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki ambaye anaitumikia klabu ya Al Ittihad ya Libya.

Aziz Ki bado yupo nchini akisikilizia hatma yake ambapo inaelezwa Yanga inafanya jitihada kubwa kumrejesha.

Nyota wengine ambao walihusishwa na Yanga ambao hata hivyo nafasi ya kusajiliwa ni finyu ni pamoja na mshambuliaji Peter Shalulile hasa baada ya Yanga hapo jana kutangaza kumsajili mshambuliaji Cheikh Ibrahima Touré.

Jean Claude Girumugisha nae alihusishwa na Yanga kwenye dirisha hili lakini ni wazi hakuna uwezekano wa kujiunga na mabingwa hao wa nchi baada ya Yanga kutangaza kuwasajili mawinga Albert Kangwanda na Housseine Zakouani.

Eneo la kiungo mkabaji Morice Chukwu raia wa Nigeria na mzawa Alphonce Mabula  wametajwa huku mshambuliaji raia wa Eswatini Justice Figuareido kutoka klabu ya Chippa United ikielezwa nae amesajiliwa.

Mashabiki wa Yanga wanasubiri kwa hamu kubaini ni nyota wepi wengine wawili wa kigeni wanakwenda kukamilisha idadi ya wachezaji 12 waliosajiliwa?

Wachezaji wa kigeni ambao wana uhakika wa kusalia kwenye kikosi cha Yanga msimu ujao ni Djigui Diarra, Yao Kouassi, Chadrack Boka, Maxi Nzengeli, Duke Abuya, Allan Okello na Laurindo Aurellio 'Depu'

Nyota hao wanaungana na Cheikh Ibrahima Touré, Housseine Zakouani na Albert Kangwanda waliosajiliwa jana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE →