Klabu ya TP Mazembe imethibitisha kuwa mlinda lango wake, Ley Matampi amemaliza mkataba wa kuitumikia timu hiyo na ameruhusiwa kuondoka baada ya kugoma kusaini mkataba mpya.
Matampi (28), mmoja wa walinda lango wa kutumainiwa wa timu ya Taifa ya DR Congo , kwa sasa ni mchezaji huru.
Alisajiliwa na TP Mazembe mwaka 2011 akitokea klabu ya AS Vital kisha Mazembe ikamtoa kwa mkopo vilabu vya Angolans Kabuscorp na DC Motema Pembe kwa nyakati tofauti.
Amekuwa chaguo la kwanza la kocha Mwinyi Zahera anayetaka amlete Yanga kuchukua nafasi ya Youthe Rostand.
Zahera ambaye yuko mapumziko DR Congo huenda akarejea na mlinda lango huyo anayesubiri kumalizana na Kamati ya usajili ya Yanga.
Yanga iko 'busy' kusaka mlinda lango baada ya kutoridhishwa na kiwango cha Youthe Rostand aliyesajiliwa msimu uliopita kutoka klabu ya African Lyon.
Benedictor Tinocco, aliyeidakia Mtibwa Sugar msimu uliomalizika ni miongoni mwa walinda lango wazawa wanaopigiwa chapuo kusajiliwa na Yanga pia.
Msimu uliomalizika Yanga ilimtegemea zaidi Rostand licha ya mapungufu yake kutokana na majeruhi ya mara kwa mara yaliyomkabili Benno Kakolanya huku Ramadhani Kabwili akikosa uzoefu.

ADVERTISE HERE