Mikakati ya kuiwinda Gor Mahia kuanza mapema

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jun 2018
Mikakati ya kuiwinda Gor Mahia kuanza mapema
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema unahitaji kuanza maandalizi mapema kuelekea mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Gor Mahia.

Mchezo huo utapigwa jijini Nairobi Julai 18, 2018 kisha timu hizo kurudiana kwenye uwanja wa Taifa Julai 29.

Baada ya kuishuhudia Gor Mahia ikitwaa taji la SportPesa Super Cup ikiwa na kikosi imara kilichoonyesha kandanda safi, Yanga inalazimika kujipanga kwelikweli kuweza kuibuka na ushindi dhidi ya wababe hao wa soka la Kenya.

Kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila ambaye alikiongoza kikosi cha Yanga kilichoondolewa kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, amesema wataanza mapema maandalizi ya kuikabili Gor Mahia.

"Tutaanza mikakati mapema kuhakikisha mchezo huo tunashinda, Gor ni timu imara tumeiona, lakini kwa muda tulionao naamini tutakuwa sawa kuwakabili," amesema Mwandila ambaye kwa sasa yuko mapumziko kwao Zambia.

Wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko ya wiki mbili na wanatarajiwa kuanza mazoezi Juni 25.

Wachezaji wa Kimataifa wanatarajiwa kurejea mapema zaidi.

Kikosi cha Yanga kinachoshiriki michuano ya CAF kitaimarika zaidi baada kuongezwa kwa wachezaji watatu ambao uongozi wa timu hiyo utawaweka hadharani hivi karibuni.

Licha ya kuanza vibaya michuano ya kombe la Shirikisho, Yanga bado ina nafasi ya kutinga robo fainali kama itapata matokeo kwenye michezo yake minne iliyobaki.

Yanga ina michezo miwili ya ugenini dhidi ya Gor Mahia na Rayon Sports huku pia ikiwa na michezo miwili ya nyumbani dhidi ya Gor Mahia na USM Alger.

USM Alger inaongza kundi D ikiwa na alama nne, inafuatiwa na Gor Mahia na Rayon Sports ambazo zote zina alama mbili wakati Yanga inashika nafasi ya mwisho kwenye kundi ikiwa na alama moja.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
32m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
57m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’