Injinia Hersi akikamilisha hizi sajili tatu wamekwisha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jul 2026
Injinia Hersi akikamilisha hizi sajili tatu wamekwisha

Jana Yanga haikutangaza sajili mpya licha ya ahadi iliyotolewa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa mabingwa hao wa nchi Ali Kamwe lakini inaelezwa kulikuwa na michakato nikubwa ya usajili iliyokuwa ikikamilishwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Said.

Yanga inataka kukamilisha michakato yote ya nyota wa kigeni kisha kuanza kuwatambulisha.

Sajili kubwa tatu

Inaelezwa kuna sajli kubwa tatu Injinia Hersi anapambana kuzikamilisha, hizi ni sajili ambazo kama zitakamilika zitamgharimu Mfadhili/Mdhamini wa Yanga Ghalib Said Mohamed 'GSM' mabilioni ya fedha.

Nyota hao ni Stephane Aziz Ki, Jean Claude Girumugisha na Peter Shalulile.

Stephane Aziz Ki

Aziz Ki bado yuko nchini akisubiri hatma yake wakati Injinia Hersi akipambana kukamilisha usajili wake licha ya dau kubwa ambalo Al Ittihad wanataka ili kumuachia.

Makubaliano ya mkataba kati ya Yanga na Aziz Ki yalishafikiwa muda mrefu, lakini Al Ittihad wamehitaji takribani Bil 1.9 ili kumuachia Aziz Ki ambaye bado ana mkataba wa miaka miwili na miamba hao wa Libya.

Aziz Ki mwenyewe tayari ameshafanya maamuzi ya kutorejea tena Libya huku pia taarifa za ndani zikibainisha pia ana mgogoro na klabu hiyo kwani hawakumaliza kumlipa fedha zake za usajili walizokubaliana wakati akitokea Wydad kujiunga na timu hiyo mwezi Januari mwaka huu.

Hivyo 'tajiri' GSM atalazimika kuweka mezani Tsh Bilioni 1.9 ili kumpata mwamba huyo kutoka Burkina Faso.

Jean Claude Girumugisha

Unaweza kusema tetesi zinazoendelea kuhusu kiungo mshambuliaji huyu wa Al Hilal ya Sudan sakata lake linafanana kabisa wakati Yanga wanamsajili Aziz Ki kwa mara ya kwanza akitoka klabu ya Asec Mimosas ya Ivory Coast mwaka 2022.

Taarifa kutoka vyanzo vingi zimebainisha kuwa MVP huyo wa ligi kuu ya Rwanda msimu uliopita tayari amesajiliwa na Al Ahli Tripoli ya Libya dau la usajili likitajwa kufikia Tsh Bilioni 13.

Lakini mpaka sasa bado timu hiyo haijamtambulisha na wakati huohuo Yanga ikiwa miongoni mwa timu zilizokuwa zikimuwania kwa ukaribu.

Inaelezwa Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alianza mapema harakati za kumvuta winga huyo Jangwani tangu mwezi March mwaka huu.

Wakala wa Girumugisha aliwahi kukiri Yanga kumuwania mteja wake wakati huo akitaja thamani yake kuwa zaidi ya dola 1.5M. 

Baada ya wachambuzi na wanahabari wengi kumaliza maneno kuwa Yanga haiwezi kumpata Girumugisha, huendi yale yaliyotokea kwa Aziz Ki mwaka 2022 yakajirudia tena kwa Girumugisha.

Peter Shalulile

Shalulile mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Namibia ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba kunako klabu ya Mamelodi Sundowns.

Yanga imetajwa kuwa miongoni mwa klabu zinahitaji hudumu yake licha ya kuwa wapo vigogo wengine kama Pyramids na Orlando Pirates.

Inaelezwa kocha mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi anamuona Shalulile kama mtu sahihi kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji kutokana na uzoefu wake.

Shalulile ndiye mfungaji bora wa muda wote ligi kuu ya Afrika Kusini akiwa na mabao 133. Manqoba alifanya kazi na mshambuliaji huyo kwa muda mrefu wakati wako Sundowns. Ni usajili mwingine unaweza kutikisa nchi kama Yanga itafanikiwa kumpata

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’