Yanga yafuata winga Comoros

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jul 2026
Yanga yafuata winga Comoros

Klabu ya Yanga inatajwa kuwa katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Housseine Zakouani kutoka Comoros.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka duru za usajili, nyota huyo anatua Yanga kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Al-Zulfi ya Saudi Arabia.

Zakouani amepita academy ya Olympique Marseille nchini Ufaransa, akiwa pia amewahi kuzitumikia klabu za Châteauroux, Hyeres 83 FC na US Thionville Lusitanos zote za Ufaransa.

Ni kiungo mshambuliaji anayemudu vyema kucheza nafasi zote za winga na hata namba 10.

Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi amehitaji kuongezewa nguvu eneo la washambuliaji wa pembeni Yanga ikihusishwa na nyota kadhaa mpaka sasa.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ameahidi kuanzia leo wataanza kutangaza majina ya nyota wa kigeni waliosajiliwa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’