Manqoba ni bingwa wa mbinu, wajiandae

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jul 2026
Manqoba ni bingwa wa mbinu, wajiandae

Mabingwa wa soka wa Tanzania Bara Yanga wameingia rasmi kwenye zama mpya wakianza maisha mapya na kocha mwenye heshima kubwa kutoka nchini Afrika Kusini, Manqoba Mngqithi.

Mngqithi anatambulika kama "Master Tactician" (Bingwa wa Mbinu), anakuja na falsafa yake maarufu ya soka la kushambulia kwa kasi, ambalo linatarajiwa kuwapa burudani ya kipekee mashabiki wa Yanga msimu huu wa 2026/2027.

Katika kuhakikisha mipango yake inafanikiwa, Kocha Mngqithi ametua nchini akiwa na jopo imara la wataalamu atakaoshirikiana nao.

Simo Dladla - Kocha Msaidizi, Kagisho Dikgacoi - Kocha Msaidizi na Mtaalamu wa Mipira ya kutenga (Set-pieces), Yardaan Valodia – Mchambuzi wa Mbinu na Viwango vya Wachezaji (Tactical Performance Analyst) na Greg Etafia – Kocha wa Makipa

Mfumo wake pendwa ni 4-3-3

Mbali na muundo wa karatasi wa 4-3-3, Kocha Manqoba Mngqithi ana namna ya pekee ya kuutafsiri mfumo huu kwa vitendo kupitia mbinu zake halisi za uwanjani. Hajengi timu inayomiliki mpira kwa ajili ya kupoteza muda, bali anatumia mfumo huo kama silaha ya kuwaangamiza wapinzani kwa kasi na akili.

Hivi ndivyo kocha huyo hujenga timu zake kulingana na nyakati tofauti za mchezo:

Wakati timu yake inapoanza kucheza kutokea nyuma, kiungo mmoja wa chini hushuka chini kabisa kukaa katikati ya mabeki wawili wa kati. Hii inaruhusu mabeki wa kando kusogea mbele haraka sana na kuwa kama mawinga.

Viungo wawili wa juu husogea kwenye "half-spaces" (maeneo yaliyo kati ya viungo wa kati na mawinga wa mpinzani) ili kupokea mipira ya haraka inayovunja mistari ya ulinzi ya adui.

Wakati timu yake inamiliki mpira kwenye robo ya mwisho ya uwanja, mfumo wa 4-3-3 hupotea kabisa. Timu inabadilika na kuwa na wachezaji watano mbele (mawinga wawili, mabeki wawili wa pembeni waliopanda, na mshambuliaji wa kati). Hii inasababisha walinzi wa mpinzani kuelemewa na idadi kubwa ya washambuliaji (overloading).

Mngqithi hupendelea mawinga wanaotumia miguu ya upande wa pili (mfano: mchezaji wa mguu wa kushoto kucheza kulia). Mbinu hii inawawezesha kukata kuelekea katikati ya uwanja (cut inside) ili kupiga mashuti au kutengeneza nafasi, huku wakiwaachia nafasi mabeki wa pembeni kupita (overlap).

Aidha, mbinu kuu ya Manqoba pindi timu inapopoteza mpira si kurudi nyuma kuzuia. Badala yake, wachezaji walio karibu na mpira wanatakiwa kuushambulia kwa nguvu ndani ya sekunde tano hadi saba za kwanza ili kuurudisha umiliki wa mpira kwao.

Katika kipindi hiki, Wananchi watarajie kuona timu yao ikicheza "high-line", yaani mabeki wa kati kusogea karibu na mstari wa katikati ya uwanja ili kupunguza nafasi ya wapinzani kupumua au kupiga pasi ndefu.

Chini yake, Wananchi watarajie kuona mabadiliko makubwa ya kiuchezaji kwa timu yao, hasa kasi ya mchezo na mikimbio ya wachezaji.

Kama kocha Sead Ramovic alivyoleta "Gusa, Achia Twende Kwao", hii ya Manqoba itakuwa: "GUSA, ACHIA TWENDE KWAO TUKAE HUKOHUKO."

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’