Leo Yanga imewatambulisha makocha wengine wanaoambatana na kocha Manqoba Mangqithi kuunda benchi la ufundi.
Simo Dladla kocha mwenye uzoefu mkubwa na soka la Afrika Kusini ametambulishwa kama kocha msaidizi huku nyota wa zamani wa Crystal Palace na Bafana Bafana, Kagiso Dikgacoi akitambulishwa kama kocha mtaalam wa mipira iliyokufa.
Yardaan Valodia akitambulishwa kama performance Analyst huku Greg Etafia akitua kama mkufunzi wa walinda lango.




ADVERTISE HERE