Wadhamini Vodacom wakabidhi vifaa timu za VPL

Yanga Damu By Yanga Damu
•
3 Aug 2017
Wadhamini Vodacom wakabidhi vifaa timu za VPL
Wadhamini wa ligi kuu ya Tanzania Bara, kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom leo imekabidhi vifaa kwa timu zitakazoshiriki ligi hiyo msimu ujao.

Akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Vodacom, Hisham Hendi amesema kwamba, kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha Ligi Kuu ya soka hapa nchini inaenda vizuri wanakabidhi vifaa vya ubora wa hali ya juu.

Hendi amesema kwamba pia Vodacom imefurahishwa na klabu zilizopanda Ligi Kuu msimu huu kutoka Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, Singida United, Lipuli na Mji Njiombe FC kuwa zimejiandaa vizuri kwa ushindani.



“Tunajisikia furaha kukabidhi vifaa hivi tukiwa tunatakeleza matakwa ya mkataba wa udhamini na ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki Ligi Kuu zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya wa Ligi,” amesema Hendi

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura ameishukuru Vodacom Tanzania na kuzitaka klabu zinazoshiriki Ligi Kuu kuzingatia na kuheshimu nembo ya mdhamini wakati wa mechi.



Wambura amesema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) halipendi kutumia kanuni na sheria kuziadhibu klabu zitazokwenda kinyume na maelekezo hayo.

Ameongeza kwamba, msimu huu wa Ligi Kuu utakuwa bora kutokana na maandalizi yote kukamilika mapema – pia timu zitakazoshiriki kuwa zimejiandaa vizuri.



Timu nyingine zinazoshiriki Ligi Kuu ni mabingwa, Yanga SC, washindi wa pili, Simba SC, wa tatu, Kagera Sugar, wa nne Azam FC, wa tano Mtibwa Sugar, wa sita Stand United, wa saba Ruvu Shooting, wa nane Tanzania Prisons, wa tisa Maji Maji, wa 10 Mwadui, wa 11 Mbeya City, wa 12 Mbao FC na wa 13 Ndanda FC
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →