Bacca, Yao wapo sana Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jul 2026
Bacca, Yao wapo sana Jangwani

Wakati ikiongeza nyota wapya katika kuimarisha kikosi, mabosi wa Yanga wako makini kuhakikisha wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza wanaendelea kusalia Jangwani.

Baada ya kufanikiwa kumbakisha nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto, beki mwingine wa kati Ibrahim Bacca nae ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kusalia kwa mabingwa hao wa soka Tanzania Bara.

Bacca na Mwamnyeto kwa sasa ndio mabeki wa kati tegemeo kwenye kikosi cha Yanga wakati huu ambao Dickson Job anaendelea kukosekana kutokana na changamoto ya majeraha.

Katika dirisha hili Yanga imeongeza beki mwingine wa kati mzawa ambaye anasubiri utambulisho. Ni Mohamed Mussa 'Yellow' kutoka klabu ya Mashujaa Fc.

Job tayari ameanza mazoezi mepesi ya kuimarisha mguu uliopata changamoto ambapo anaweza kurejea kikamilifu mwezi Novemba.

Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kuongeza mkataba kwa mlinzi wa kulia Yao Kouassi ambaye sasa yuko fit kwa asilimia 100 baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa sehemu kubwa ya msimu uliopita.

Mpaka sasa ni Prince Dube pekee aliyeondoka ambaye hata hivyo aliomba arejee kwao Zimbabwe kwa mahitaji yake binafsi ili kuwa karibu na familia yake.

Lakini nyota wengine wote ambao wako kwenye mipango ya Yanga kuelekea msimu ujao, wataendelea kusalia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
36m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
4h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
9h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’