Ratiba ya ligi kuu 2026/27 imetangazwa rasmi leo ambapo mabingwa watetezi Yanga wanaanzia ugenini kwa mchezo dhidi ya Namungo Fc utakaopigwa Agosti 15 uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo baada ya kumalizana na Namungo Fc, mabingwa hao wa nchi watarejea Dar es saaam kwenye uwanja wa nyumbani (Uhuru) ambapo watacheza mechi tatu dhidi ya Coastal Union (Agosti 20), JKT Tanzania (Agosti 24) na Pamba Jiji (Agosti 28).
Septemba 1 Wananchi watakuwa mkoani Arusha kuikabili Fountain Gate uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Kariakoo Derby
Mchezo wa mapema kukaribisha msimu kati ya Yanga dhidi ya Simba utapigwa Agosti 12 Ngao ya Jamii kabla ya timu hizo kukutana Oktoba 10 mchezo wa duru ya kwanza Simba wakiwa wenyeji na Februari 06 mchezo wa duru ya pili Yanga wakiwa wenyeji ligi kuu.
Ratiba kamili itapatikana ndani ya Mwana Jangwani..