Hatma ya wiki ya Mwananchi kufahamika wiki hii

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jul 2026
Hatma ya wiki ya Mwananchi kufahamika wiki hii

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema hadi kufikia Julai 20 siku ambayo kikosi cha Yanga kitaingia kambini, watakuwa wametangaza wapi Wiki ya Mwananchi itafanyika mwaka huu 2026.

Baada ya uwanja wa Benjamin Mkapa kufungwa kutokana na ukarabati unaoendelea, kumekuwa na changamoto ya kupata kiwanja kikubwa cha kufanya Tamasha hilo.

Aidha Kamwe amesema pia wamepokea mialiko kutoka nchi mbalimbali ambazo zingependa Tamasha hilo liandaliwe.

"Mpaka sasa bado tunaendelea kufanya tathmini lakini mpaka kufikia Julai 20 tutakuwa tumepata majibu"

"Sote tunafahamu uwanja wa Benjamin Mkapa umefungwa kutokana na ukarabati unaoendelea hivyo tunapaswa kuamua wapi tukafanye Tamasha letu"

"Tumepokea mialiko kutoka nchi mbalimbali ambazo zingependa tukafanye Tamasha letu, ndani ya siku hizi chache tutakuwa na majibu"

"Kuhusu uzinduzi mpaka sasa imependekezwa mkoani Geita, Katoro lakini bado tunapokea maoni," alisema Kamwe.

Shamrashamra za kilele cha Wiki ya Mwananchi huenda zikafanyika mwanzoni mwa mwezi Agosti.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’