Mshambuliaji wa Yanga Emmanuel Mwanengo anatarajiwa kujiunga Singida BS kwa mkopo wa msimu mzima, imefahamika.
Inaelezwa tayari walima alizeti hao wamefikia makubaliano na Yanga kwa ajili ya mchezaji huyo ambaye alitua kwa Wananchi kwenye usajili wa dirisha dogo.
Licha ya kutua Jangwani akiwa na matarajio makubwa, Mwanengo ameshindwa kuonyesha ushawishi na kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
Mwanengo alitua Jangwani akitokea klabu ya TRA United ambayo aliitumikia kwa muda mfupi akijiunga nayo akitoka kucheza soka la kulipwa nchini Tajikistan katika klabu ya Vakhsh Bokhtar.
ADVERTISE HERE