Kiungo mshambuliaji wa Fountain Gate Juma Abushiri 'Chuga Boy' tayari yuko jijini Dar es salaam akisubiri kutambulishwa rasmi na mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga.
Chuga alipaswa kusafiri kuelekea Ubelgiji siku ya jana Julai 12 kwenda kufanya majaribio kunako klabu ya KAA Genk hata hivyo mpango huo umekufa rasmi baada ya winga huyo kuuambia uongozi wa Fountain Gate kuwa ameamua kujiunga na Yanga.
Chuga alikuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya vijana ambapo baada ya kuvunjwa kambi sasa kituo chake kinachofuata ni Jangwani.
Kinda huyo amepata baraka zote kutoka kwa wazazi wake ili awatumikie Wananchi. Yanga imeridhia kununua muda wa mkataba wake uliokuwa umesalia na klabu ya Fountain Gate ili kumruhusu kinda huyo akatimize ndoto yake pale mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam.
Yanga imempa Chuga mkataba wa miaka mitatu ambao unajumuisha mshahara mnono na pesa ya usajili.
Dili la Chuga lilikamilisha wiki iliyopita na mmoja wa viongozi waandamizi wa Yanga ambapo alifunga safari kuonana na Wazazi wa kinda huyo ambao kimsingi walitoa baraka zote akaitumikie Yanga.