Aziz Ki awapa matumaini mashabiki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jul 2026
Aziz Ki awapa matumaini mashabiki Yanga

Baada ya kuonekana mkoani Morogoro juzi kwenye Tamasha la Wape Tabasamu, kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki amewapa matumaini mashabiki wa Yanga juu ya urejeo wake Jangwani.

Aziz Ki alishiriki Tamasha hilo la kurejesha kwa Jamii lililoandaliwa na wachezaji wa Yanga Kibwana Shomari, Dickson Job na Aboutwalib Mshery akiitumikia timu Kibwana.

Akizungumza na wanahabari kwa ufupi baada ya mchezo huo, pale alipoulizwa juu tetesi zinazomuhusisha kurejea Yanga, Aziz Ki alijibu kwa ufupi 'Inshallah' akimaanisha kwa uwezo wa Mwenye ez Mungu inawezekana.

Yanga tayari ina makubaliano binafsi na Aziz Ki kurejea kwa mabingwa hao wa nchi huku Aziz Ki akiwa amewataarifu waajiri wake Al Ittihad juu ya uamuzi wake wa kuondoka.

Hata hivyo kuna makubaliano ambayo yanapaswa kufikiwa kati ya Aziz Ki na Al Ittihad kabla ya Yanga kukamilisha usajili wake.

Al Ittihad iko kwenye presha kubwa kutokana na mastaa wake wa kigeni kuachana na timu hiyo kwa kile kinachoelezwa kuzorota kwa hali ya kiusalama nchini humo.

Hata kocha Rulani Mokwena aliyejiunga na timu hiyo mwezi Januari nae amevunja mkataba wake akitimkia Pyramids ya Misri.

Aziz Ki ameshafanya maamuzi ya kutorejea tena kunako klabu hiyo, suala la kurejea Jangwani unaweza kusema ni muda tu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’