Klabu ya Al Ittihad ya Libya inatajwa kumuwania kocha wa viungo wa klabu ya Yanga Tshephang Mokaila, imefahamika.
Mokaila amemaliza mkataba wa mwaka mmoja aliosaini msimu uliopita nae akisubiri hatma yake.
Uongozi wa Yanga bado uko kwenye mchakato wa kusaka kocha mkuu ambaye atapewa nafasi ya kupendekeza wataalam anaohitaji kuendelea nao kwenye benchi lake.
Mokaila amekuwa na nyakati nzuri kwenye kikosi cha Yanga, alikuwa sehemu ya benchi la ufundi lililoundwa na kocha Romain Folz ambaye alifutwa kazi mwanzoni mwa msimu uliopita.
Kazi yake imeonekana zaidi kwenye mechi za mwishoni mwa msimu kwani licha ya ratiba ngumu, alihakikisha wachezaji wanakuwa kwenye utimamu wa mwili na hatimaye Yanga kufanikiwa kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo.
Yanga iliweza kushinda mechi 6 kati ya 7 za mwisho ikizifunga Singida BS 3-0, Azam Fc 3-0, TRA United 3-0 na JKT Tanzania 3-0 katika mechi ambazo wengi waliamini Yanga ingedondosha alama na kupoteza ubingwa wa ligi kuu