Baada ya kipindi kigumu cha majeraha, habari njema kwa Wananchi ni kuwa nyota wao beki Dickson Job na mshambuliaji Clement Mzize wako mbioni kurejea kikosini.
Mzize na Job tayari walishaanza mazoezi mepesi na pengine huenda wakaungana na wachezaji wenzao wakati wa pre-season ya maandalizi ya msimu ujao.

Wakati Mzize na Job wakitarajiwa kurejea, Yanga itaendelea kumkosa Pacome Zouzoua ambaye amefanyiwa upasuaji wa jeraha alilopata kwenye mchezo wa mwisho msimu uliopita dhidi ya JKT Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa awali na Yanga, Pacome atakuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa kipindi cha wiki sita ambapo baada ya muda huo, itafahamika muda ambao atakuwa nje hadi kupona majeraha yake. Kutokana na aina ya jeraha lake, huenda akakosekana kwa miezi kadhaa.
Wachezaji wa Yanga wanatarajiwa kurejea kambini mwishoni mwa mwezi huu kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao 2026/27.