Yanga yajitosa kumuwania winga Sekhukhune United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jul 2026
Yanga yajitosa kumuwania winga Sekhukhune United

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, wameanza harakati za kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu mpya kwa kufungua mazungumzo ya kumuwania winga wa kushoto wa Sekhukhune United ya Afrika Kusini, Keletso Makgalwa.

Makgalwa mwenye umri wa miaka 29 amekuwa mmoja wa wachezaji waliovutia zaidi katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini (Betway Premiership) kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutengeneza nafasi za mabao, kasi akiwa pembeni na ubora wake katika mashambulizi ya kushtukiza. Taarifa kutoka Afrika Kusini zinaeleza kuwa nyota huyo yuko tayari kupokea changamoto mpya nje ya nchi yake, jambo lililoifanya Yanga kuanza mchakato wa kumshawishi kujiunga na kikosi hicho.

Vyanzo vinaeleza kuwa Yanga tayari imeanzisha mawasiliano na Sekhukhune United kuhusu uwezekano wa kufanya biashara hiyo, ingawa hadi sasa hakuna ofa rasmi iliyowasilishwa. Simba pia imeonyesha nia ya kumfuatilia mchezaji huyo, lakini taarifa zinaonyesha Yanga ndiyo iliyopiga hatua zaidi katika mazungumzo ya awali.

Kocha wa Sekhukhune United, Eric Tinkler, amewahi kuweka wazi kuwa klabu hiyo iko tayari kumuuza Makgalwa iwapo itapokea ofa inayokidhi thamani waliyoiweka kwa mchezaji huyo, hali inayofungua mlango kwa klabu zinazomhitaji kuingia mezani kwa mazungumzo rasmi.

Makgalwa alikuwa na msimu bora wa 2024/25 baada ya kufunga mabao sita na kutoa asisti 11 katika mechi 32 za mashindano yote, kiwango kilichomfanya ateuliwe kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu pamoja na tuzo ya Wachezaji Bora iliyopigiwa kura na wachezaji wenzake nchini Afrika Kusini.

Katika msimu uliopita aliendelea kuwa miongoni mwa wachezaji wenye ushawishi mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji ya Sekhukhune United, akitajwa kama mmoja wa vinara wa kutengeneza nafasi nyingi za mabao na kutoa asisti katika Betway Premiership.

Makgalwa si mchezaji mgeni kwenye soka la Afrika Kusini. Kabla ya kujiunga na Sekhukhune United aliwahi kuzichezea Mamelodi Sundowns, TS Galaxy, Moroka Swallows na Upington City, ambako alifanikiwa kufufua kiwango chake kabla ya kurejea ligi kuu na kuwa mmoja wa wachezaji wanaotafutwa zaidi kwa sasa.

Iwapo dili hilo litakamilika, Makgalwa atakuwa nyongeza muhimu kwa Yanga kutokana na uwezo wake wa kucheza winga wa kushoto, kulia pamoja na kushambulia kutoka maeneo ya kati.

Kasi yake, ubunifu na uwezo wa kutengeneza nafasi vinaweza kuipa Yanga nguvu mpya katika mashindano ya ndani na kimataifa msimu ujao.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’