Mashabiki na Wanachama wa Yanga leo wataungana na wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wao katika shamrashamra za kusherehekea ubingwa wa 32 ligi kuu ya Tanzania Bara.
Shamra shamra za mwaka huu zitakuwa za aina yake kwani Wananchi watasherehekea ubingwa wa tano mfululizo kwa kufanya paredi la aina yake.
Paredi hilo litaanzia Karume kupita Msimbazi na kuelekea Makao Makuu ya Yanga, Jangwani ambako kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.

Ni kuanzia saa 4 asubuhi..!
ADVERTISE HERE