Rais wa Yanga injinia Hersi Said jana amewaongoza mashabiki na wanachama wa Yanga kufika dukani kwa beki Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' na kujipatia perfume'
Injinia Hersi alifanya manunuzi pamoja na kuwakaribisha Wananchi wote kumsapoti beki huyo aliyetua Yanga msimu uliopita akitokea klabu ya Simba. Huu umekuwa kama utaratibu kwa Yanga wakifanya hivyo kila mwisho wa msimu.
Msimu uliopita Wananchi walitembelea duka la nguo la mshambuliaji Clement Mzize na kujipatia mahitaji yao.
Kocha Mkuu wa Yanga Abdihamid Moalin, Meneja Walter Harrison, Msemaji Ali Kamwe na maafisa wengine wa Yanga walifika dukani hapo.



ADVERTISE HERE