Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema mshamuliaji Prince Dube aliyejiunga na klabu ya Hardrock Fc ya kwao Zimbabwe, hakushawishiwa na pesa kujiunga na timu hiyo.
Kamwe amesema Yanga ilikuwa tayari kumbakisha mshambuliaji huyo lakini yeye mwenyewe aliomba arejee kucheza soka la nyumbani.
Msemaji huyo wa mabingwa wa soka Tanzania Bara 2025/26, ameongeza kuwa Dube alikuwa na ofa nono zaidi kutoka nchi za Libya, Afrika Kusini na Morocco lakini ulikuwa ni uamuzi wake kurejea Zimbabwe.
"Dube amehitaji mwenyewe kurudi kwao Zimbabwe, Yanga ilianza kufanya mchakato muda mrefu wa kutaka kumuongezea mkataba."
"Yanga ilikuwa tayari kumbakisha ila Dube naye alikuwa na mawazo yake ambayo alihitaji asikilizwe ya kwamba kwa sasa anatamani kurudi kucheza soka nyumbani kwao."
"Maamuzi ya kuondoka Yanga hayakuchochewa na pesa kwasababu alikuwa na ofa kubwa sana nchini Libya yenye pesa ndefu, Afrika kusini na hata Morocco kwenye timu ya Raja Casablanca inayofundishwa na Nabi ila zote hizo alizikataa na kuamua kurudi nyumbani kwao."
"Kwa mawazo yake hayo, basi uongozi haukuwa na namna nyingine ya kufanya kwasababu mchezaji huyo aliamua moja kwa moja kurudi kwao," alisema Kamwe.
Dube alitambulishwa na klabu ya Hardrock Fc ya Zimbabwe jana baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga