Paul Matthews arejea Afrika Kusini, atua Marumo Gallants

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jul 2026
Paul Matthews arejea Afrika Kusini, atua Marumo Gallants

Aliyekuwa Mkurugenzi wa ufundi wa Yanga SC, Paul Matthews, amerejea rasmi nchini Afrika Kusini baada ya kutangazwa kuwa Sporting Director mpya wa klabu ya Marumo Gallants kuelekea maandalizi ya msimu wa 2026/27.

Matthews anaondoka Yanga baada ya kuhudumu kwa msimu mmoja, ambapo alikuwa na jukumu la kusimamia masuala ya kiufundi ya klabu, ikiwemo mipango ya maendeleo ya kikosi, usajili wa wachezaji pamoja na ukuzaji wa vipaji vya vijana.

Kabla ya kujiunga na Yanga mwaka 2025, Matthews alikuwa miongoni mwa wataalamu waliokuwa na heshima kubwa katika soka la Afrika Kusini.

Aliwahi kufanya kazi katika klabu za SuperSport United, AmaTuks, Jomo Cosmos na Tembisa Classic, akijenga sifa kupitia uwezo wake wa kutambua vipaji, kusimamia usajili wa wachezaji na kuweka mifumo ya maendeleo ya vijana.

Akiwa Yanga, Matthews alikuwa sehemu ya maboresho ya idara ya ufundi na usajili, akifanya kazi kwa karibu na uongozi wa klabu katika kuhakikisha kikosi kinakuwa na ushindani mkubwa kwenye mashindano ya ndani na kimataifa.

Amesimamia kuanzishwa mradi wa Shule ya soka ya Yanga ambapo kwa sasa vijana wameendelea kuandaliwa kwenye Shukle 

Kuondoka kwa Matthews kunamaanisha Yanga italazimika kutafuta mbadala wa nafasi hiyo muhimu katika kipindi hiki ambacho ligi imemalizika.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
26m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’