Sure Boy utumishi wa heshima Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Jul 2026
Sure Boy utumishi wa heshima Yanga

Kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' amemaliza mkataba wa kuwatumikia mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga.

Kiungo huyo mkongwe alijiunga na Yanga SC mwezi Desemba 2021, usajili wake ulikamilika baada ya yeye mwenyewe kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake na klabu yake ya zamani ya Azam FC, aliyoidumu kwa takriban miaka 14.

Haikuwa rahisi kwa Azam Fc kumruhusu Sure Boy atue kwa Wananchi kwa sababu alikuwa bado mchezaji muhimu na wakati huo ushindani kati ya Yanga na Azam Fc ndio ulikuwa umeanza kushamiri.

Baada ya Yanga kuwasajili Mudathir Yahya na Sure Boy ndipo Azam Fc nao wakajibu kwa Feisal Salum 'Fei Toto' kabla ya Yanga kurudi tena kumchukua Prince Dube. Awali Azam Fc pia iliwasajili Frank Domayo na Didier Kavumbagu huku Yanga ikimsajili Gadiel Michael.

Sure Boy ameitumikia Yanga kwa takribani msimu minne akifanikiwa kushinda mataji matano ya ligi kuu, matatu ya kombe la CRDB, Ngao ya Jamii bila ya kusahau kucheza fainali ya kombe la Shirikisho la CAF (CAF CC) katika msimu ambao alikuwa nguzo muhimu kwenye michuano hiyo hasa baada ya Khalid Aucho kukosekana.

Ni wazi Sure Boy anaondoka Yanga na heshima kubwa, kwani hata katika nyakati ambazo alikuwa haonekani uwanjani, alitumia ukongwe na uzoefu wake katika vyumba vya kubadilishia nguo kwa kuwaongezea wenzake hamasa na ari ya kupambana.

Klabu ya JKT Tanzania inatajwa kuwania saini ya mkongwe huyo ambaye historia yake na Yanga imeanza mbali.

Sure Boy ni jina ambalo alipewa Baba yake Aboubakar Salum aliyekuwa winga hatari wa Yanga mwishoni mwa miaka ya 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’