Uongozi wa JKT Tanzania na mchezaji Hassan Wahabi wamemtembelea kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua aliyelazwa Hospitali ya Agha Khan baada ya kufanyiwa upasuaji.
Pacome alipata jeraha katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kati ya JKT Tanzania FC na Yanga SC, uliochezwa tarehe 30 Juni 2025 kwenye Uwanja wa Major General Isamuhyo, baada ya kugongana na mchezaji Hassan Wahabi walipokuwa wakiwania mpira.
Mapema leo, Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent IbengΓ©, akiwa ameambatana na wajumbe wa benchi la ufundi la klabu hiyo, walifika hospitalini hapo kumjulia hali Pacome. Katika ziara hiyo, Ibenge aliambatana na Kocha Msaidizi, Anicet Kiazayidi na Kocha wa Makipa, Rody Mountaro.


Get well soon Pacome..!
ADVERTISE HERE