Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema shamrashamra za kushangilia ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo zitafanyika Jumamosi hii, Julai 04.
Kamwe amesea awali ilipangwa paredi hilo lifanyike jijini Mwanza pekee ila baada ya kushauriana, paredi hiyo itaanzia Mwanza na kuhitimishwa Dar es Salaam, Jangwani kama walivyofanya miaka yote.
Kamwe amedokeza kuwa nahodha wa zamani wa Simba Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' ndiye atakayeongoza shamrashamra kwenye gari maalum ambapo pale mitaa ya Msimbazi yalipo Makao Makuu ya waajiri wake wa zamani, atakuwa na jambo lake!
Huu utakuwa ubingwa wa tano mfululizo Yanga inafanya paredi wakati huu wakiongeza wigo shamrashamra zikianzia mkoani na kuhitimishwa Dar es salaam.
ADVERTISE HERE