Pacome afanyiwa upasuaji Agha Khan

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jul 2026
Pacome afanyiwa upasuaji Agha Khan

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametoa taarifa kuhusu hali ya mchezaji Pacome Zouzoua ambaye jana alipata majeraha yaliyomfanya akimbizwe Hospitalini kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.

Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 na kutwaa taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo. Hata hivyo kuumia kwa Pacome kuliacha simanzi kwa Wanayanga.

Akizungumza na wanahabari mapema leo, Kamwe alisema baada ya kuumia, Pacome alikimbizwa Hospitali ya Akha Khan jijini Dar es salaam ambapo baada ya mashauriano ya madaktari mchezaji huyo akafanyiwa upasuaji uliokwenda sawa kwa asilimia 100.

"Mchezaji wetu Pacome Zouzoua, baada ya kutolewa jana uwanjani kwa msaada wa Ambulance, alipelekwa moja kwa moja kwenye hospitali ya Akha Khan."

"Kwa sababu ya jeraha lake kuwa baya, akaingia moja kwa moja kitengo cha dharura ambapo Madaktari pale Agha Khan na wa klabu yetu (Yanga), wakakubaliana kwamba jeraha iile halitakiwi kucheleweshwa kupatiwa matibabu"

"Hivyo baada ya majadiliano, uongozi ukatoa baraka zake, Pacome Zouzoua afanyiwe upasuaji jana kwa ajili ya kupatiwa matibabu, tunamshukuru Mungu majira ya saa 8 usiku upasuaji ulikamilika kwa mafanikio ya asilimia 100"

"Kwa mujibu wa ripoti ya madaktari, watakuwa na wiki 6 za kumuangalia baada ya upasuaji ambao ni uangalizi wa awali.Baada ya muda huo klabu itakuwa kwenye nafasi ya kuwaambia Pacome atakuwa nje kwa muda gani."

"Najua Wanayanga wengi jana mlikuwa na mchanganyiko wa mawazo. Tulikuwa na furaha kwa kuwa tumetetea ubingwa wetu lakini ndani ya mioyo yetu tulikuwa na simanzi kwa sababu Mwanajeshi wetu mmoja ambaye tangia ameanza kuvaa jezi ya klabu yetu alikuwa anajitoa kwa asilimia 100 kuhakikisha klabu yetu inapata mafanikio."

"Ilituumiza sana, wakati wa mapumziko vilio vilitawala kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, nichukue fursa hii kumpongeza sana Salum Aboubakar 'Sure Boy' ambaye alifanya kazi kubwa kuhakikisha anazungumza na wachezaji wenzake, kuwaweka sawa na hatimaye kurudi uwanjani wakiwa sawa kukamilisha kipindi cha pili," alisema Kamwe.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’