Yanga haijaanza leo kumuwania Kagere

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jun 2018
Yanga haijaanza leo kumuwania Kagere
Tetesi za mshambuliaji tegemeo wa Gor Mahia, Meeddy Kagere kuwaniwa na Yanga zimezidi kushika kasi.

Tetesi hizo zimepamba moto wakati huu baada ya kubainika kuwa mshambuliaji huyo anamaliza mkataba wa kuitumikia Gor Mahia mwezi ujao na mwenyewe yuko tayari kuondoka klabuni hapo kama atapata ofa ya maana.

Gazeti la Mwanaspoti limedai kufanya mahojiano na mshambuliaji huyo mkongwe wakati wa michuano ya SportPesa aliyoibuka mfungaji bora kwa msimu wa pili mfululizo na kukiri anaweza kutua Yanga kama atatimiziwa mahitaji yake.

Hii sio mara ya kwanza kwa Yanga kumuwania Kagere raia wa Rwanda ambaye ni mzaliwa wa Uganda.

Mwaka 2012 Marcio Maximo alipojiunga na Yanga alijaribu kumsajili Kagere wakati huo akichezea klabu ya Polisi inayoshiriki ligi kuu ya Rwanda.

Kagere pia alihusishwa na kusajiliwa Yanga msimu uliopita baada ya kumalizika kwa mashindano ya SportPesa Super Cup ambayo nayo aliibuka mfungaji bora.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alikiri kufanya mazungumzo na mshambuliaji huyo mwaka jana.

Licha ya kocha wa Gor Mahia Dylan Kerr kusisitiza kuwa bado mshambuliaji huyo yuko kwenye mipango yake, Kagere hajasaini mkataba mpya na ametoa nafasi kwa timu zinazotaka huduma yake kufika mezani.

Kamati iliyoundwa na klabu ya Yanga kusimamia masuala ya usajili na mikataba ya wachezjai imeahidi kusajili wachezaji wenye hadhi ya juu ili kuirejeshea Yanga makali yake.

Hata hivyo kama Yanga itaweza kumnasa Kagere hatakuwa na sifa ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho kwa kuwa tayari ameitumikia Gor Mahia kwenye michuano hiyo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
9h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
13h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
14h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
14h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’