JKT Tanzania waomba radhi, watoa pole kwa Pacome

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jul 2026
JKT Tanzania waomba radhi, watoa pole kwa Pacome

Uongozi wa klabu ya JKT Tanzania umeomba radhi kufuatia tukio la mchezaji wa timu hiyo Hassan Wahabi kumfanyia rafu mbaya kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua.

Taarifa iliyotolewa na JKT Tanzania mapema leo, imebainisha kuwa tukio hilo halikuwa la kimakusudi.

"Uongozi wa JKT Tanzania FC, umehuzunishwa na tukio la kuumia kwa mchezaji wa Yanga SC, Pacome Zouzoua aliyeumizwa na mchezaji Hassan Wahabi, wakati wakiwania mpira, katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, JKT Tanzania FC Vs Yanga SC, uliochezwa katika uwanja wa Major General Isamuhyo, 30 June 2025.

Kwa niaba ya mchezaji wa timu ya JKT Tanzania FC, Hassan Wahabi, uongozi tunaomba radhi kwa tukio hilo, ambalo halikuwa la kimakusudi, lililomsababishia maumivu makali Pacome Zouzoua, linalomtesa na kumuumiza kifikra mchezaji wetu Wahabi, kutokana na maumivu aliyoyapata Zouzoua, ambayo hakuyakusudia wala kuyatarajia.

Aidha, uongozi wa JKT Tanzania FC, tunatoa pole ya dhati kwa mchezaji Zouzoua, tunamuombea kwa mwenyezi Mungu, apone haraka na arejea katika hali yake ya kawaida, acheze mpira katika kiwango na ubora wake wa siku zote."

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’