Juzi Mdhamini/Mfadhili wa Yanga Gharib Said Mohamed 'GSM' alikuwepo dimba la KMC Complex wakati Yanga ikiiadhibu TRA United mabao 3-0 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo.
GSM alionekana jukwaa kuu akiwa sambamba na Rais wa Yanga Injinia Hersi Said, Makamu wa Rais Arafat Haji, Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini na muasisi wa vuguvugu la Yanga mpya akiandaa Tamasha la Kubwa Kuliko ambalo ndio lilileta Udhamini wa GSM Yanga.
Kesho Jumanne, Yanga inakwenda kuhitimisha msimu uwanja wa Isamuhyo dhidi ya JKT Tanzania mchezo utakaopigwa saa 10 jioni.
Kwa mara nyingine, GSM anatarajiwa kuongoza mapambano pale Isamuhyo kuhakikisha Yanga inatwaa ubingwa.
GSM hajawahi kuwa na maneno mengi, kauli yake ni moja tu YANGA BINGWA bila shaka kesho kauli hiyo itatimia kwa mara nyingine.